Ujerumani yaitambia Australia kombe la mabara

Conf Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Ujerumani na Australia wakipongezana baada ya mchezo kumalizika

Timu ya taifa ya Ujerumani imeichapa timu ya Australia kwa mabao 3-2 katika mchezo wa kundi wa kombe la mabara michuano inayofanyika huko nchini Urusi.

Iliwachukua dakika tano tu kwa Ujerumani kuandika bao la kwanza kupitaia mshambuliaji wa ke Lars Stindl, Australia wakasawazisha goli hilo katika dakika ya 41 kwa goli la Tom Rogic.

Mshambuliaji matata wa Ujerumani Julian Draxler akaongeza goli la pili kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 45.

Dakika ya 48 Ujerumani waliongeza bao la tatu kupitia kwa kiungo Leon Goretzka, goli la pili la Austaria lilifungwa na mshambuliaji Tomi Juric anayekipiga katika klabu ya FC Luzern.