Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 20.06.2017 na Salim Kikeke

Alex Oxlade-Chamberlain Haki miliki ya picha PA

Chelsea wanajiandaa kuingia katika mbio za kutaka kumsajili Alex- Oxlade Chamberlain kutoka Arsenal, huku Liverpool na Manchester City wakimnyatia kiungo huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 23 (Mirror).

Nemanja Matic, 28, anataka kwenda Manchester United kuungana na meneja wake wa zamani Jose Mourinho (Sun).

Manchester City wanajiandaa kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre- Emerick Aubameyang, 28 (Sky Sports).

Hata hivyo taarifa nyingine zinasema Manchester City hawana mpango wa kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang (Express).

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, hatadai mshahara mkubwa ili kuhakikisha anaweza kuhamia Manchester United (Sun).

Manchester United hawana uhakika kama wanataka kumsajili Ronaldo (Daily Express).

Image caption Bei ya Cristiano Ronaldo inakadiriwa kuwa pauni milioni 350

Jose Mourinho amesema hataki kumsajili Ronaldo (Daily Star).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana wasiwasi kuwa huenda Cristiano Ronaldo anaitumia United ili kujipatia mkataba mpya Real Madrid (The Express).

Manchester United watarejea tena na dau jipya kutaka kumsajili Nelson Semedo kutoka Benfica (O Jogo).

Antonio Conte atakuwa na mazungumzo na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovic, huku Chelsea wakiwa na matumaini Muitaliano huyo ataongeza mkataba wake (Telegraph).

Antonio Conte anakaribia kusaini mkataba mpya Chelsea (Sky Italia).

Chelsea wapo tayari kumuongezea mkataba Conte na kumuongezea mshahara wa kufikia pauni milioni 9.5 kwa mwaka (Daily Mail).

West Ham huenda wakakabiliwa na upinzani kutoka kwa Manchester United kumwania kipa wa Manchester City Joe Hart, 30 (Telegraph).

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mohamed Salah alifungia Roma mabao 15 mechi 31 Serie A msimu wa 2016-17

Southampton watazungumza na kocha wa zamani wa Alaves, Mauricio Pellegrino na huenda wakamtagaza meneja mpya mwishoni mwa wiki hii (ESPN).

Dani Alves ameiambia Juventus kuwa anataka kuondoka na kwenda kuungana na meneja wake wa zamani Pep Guardiola (Guardian).

Juventus wamezungumza na Dani Alves kuhusu kuuvunja mkataba wake, huku wawakilishi wa mchezaji huyo wakizungumza na Manchester City na Chelsea kutazama uwezekano wa uhamisho wa beki huyo kutoka Brazil (Daily Mail).

Barcelona wanataka kuvunja rekodi ya usajili kwa kupanda dau kumsajili nyota wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele (Bild).

Swansea wamezungumza na beki wa zamani wa Chelsea John Terry, 36, na wana matumaini nahodha huyo wa zamani wa England atakubali kujiunga nao msimu ujao (Mirror).

Mohamed Salah, 25, anasubiri kuitwa Liverpool ili kwenda kukamilisha uhamisho wake kutoka Roma, ingawa hakuna tarehe iliyopangwa ya kufikia makubaliano ya usajili huo (Liverpool Echo).

Newcastle watakamilisha mkataba wa pauni milioni 9 kumsajili mshambiliaji wa kimataifa wa Cameroon Vincent Aboubakar, 25, anayechezea Porto, na pia watatoa pauni milioni 8.7 kumsajili beki wa Eibar, Florian Lejeune, 26 (Daily Star).

Juventus wameungana na Liverpool na Chelsea katika mbio za kutaka kumsajili Ruben Neves kutoka Porto (Mirror).

Lyon wana uhakika wa kukamilisha usajili wa pauni milioni 16.6 wa Bertrand Traore kutoka Chelsea (Evening Standard).

Roma wameanza mazungumzo na Feyenoord kwa ajili ya kumsajili beki wa kulia Rick Karsdrop (Voetbal International).

Beki wa Barcelona Jeremy Mathieu amesafiri kwenda Ureno kukamilisha uhamisho wake kwenda Sporting Lisbon (A Bola).

Bayern Munich wanataka kumsajili beki wa Tottenham Kyle Walker (The Sun).

Mshambuliaji wa Arsenal Takuma Asano atabakia Stuttgart kwa mkopo kwa msimu mmoja zaidi (Bild).

Arsenal wanajiandaa kutoa euro milioni 30 kumsajili kiungo Arda Turan kutoka Barcelona (Goal.com).

Miralem Pjanic huenda akasajiliwa na Barcelona iwapo klabu hiyo itashindwa kumchukua Marco Verratti (Mundo Deportivo).

Kylian Mbappe ameweka wazi kwa Monaco kuwa anataka kujiunga na Real Madrid (Marca).

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kylian Mbappe akifungia Monaco dhidi ya Lyon katika Ligue 1 Aprili

Tottenham wako tayari kupambana na Arsenal katika kumsajili beki wa Manchester United Chris Smalling (The Sun).

Barcelona wanajiandaa kuwapa Arsenal Rafinha Alcantara na pauni milioni 20 juu ili kubadilishana na Hector Bellerin (Marca).

Borussia Dortmund wanapanga kutaka kumsajili Lee Seung-Woo kutoka Barcelona (Bild).

AC Milan wanataka kumsajili Bernd Leno, 25, kutoka Bayer Leverkusen, ili kuziba nafasi ya kipa Gianluigi Donnarumma (Bild).

Manchester United na Bayern Munich wanamfuatilia Karamoko Dembele, 14, anayechezea Celtic (the Sun).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Mada zinazohusiana