Jose Mourinho adaiwa kukwepa kodi Uhispania

Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametuhumiwa kufanya ulaghai wakati wa ulipaji kodi alipokuwa katika klabu ya Real Madrid.

Maafisa wa mashtaka nchini humo wanasema alitenda makosa hayo alipokuwa mkufunzi mkuu wa klabu hiyo.

Anatuhumiwa kukwepa kolipa kodi ya jumla ya €3.3m (£2.9m; $3.6m) kati ya mwaka 2011 na mwaka 2012.

Bado hajazungumzia madai hayo.

Watu wengine mashuhuri aktika soka ambao wametuhumiwa kufanya ulaghai wakati wa kulipa kodi Uhispania majuzi ni pamoja na nyota wa Barcelona Lionel Messi, ambaye alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 jela.

Hata hivyo Messi, hatarajiwi kwenda jela.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii