Murray, Warrinka watupwa nje michuano ya Aegon

TENESI Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jordan Thompson na Andy Murray baada ya mchezo kumalizika

Bingwa mtetezi wa michuano ya tenesi ya Aegon Muingereza Andy Murray, ametupwa nje ya michuano hiyo na mchezaji namba 90 kwa ubora wa mchezo huo Jordan Thompson.

Murray anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya tenesi alifungwa kwa 7-6 (7-4) 6-2.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jordan Thompson akishnaglia ushindi wake dhidi ya Andy Murray

Stan Warrinka nae alitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuchapwa na Feliciano Lopez kwa seti mbili alizopoteza kwa 7-6 na 7-5.

Nyota mwingine aliyeondolewa kwenye michuano hiyo ni Milos Raonic aliyefungwa na Thanasi Kokkinakis kwa seti mbili ya 7-6 na 7-6.