Azarenka aanza vibaya michuano ya tenesi ya Mallorca

tenesi Haki miliki ya picha Google
Image caption Victoria Azarenka

Mcheza tenesi Victoria Azarenka amerejea uwanjani na kuanza vibaya baada kushindwa kutamba mbele ya Mjapani, Risa Ozaki, na ukiwa ndio mchezo wa kwanza kwa Azarenka, baada ya kuwa nje ya mchezo kwa muda wa mwaka mmoja.

Azarenka ambae hajacheza toka mwaka 2016, mara ya mwisho alishiriki michuano ya wazi ya Ufaransa, alianza vizuri mchezo dhidi ya Ozaki, ambapo aliongoza kwa 6-3 kabla ya kupoteza kwa 6-4, 5-4 katika mchezo wa raundi ya kwanza.

Mcheza tenesi huyu alipumzika kwa muda kucheza mchezo huo baada ya kujifungua mtoto mnamo mwezi Desemba mwaka jana.

Azarenka baada ya michuano ya Mallorca atashiriki michuano ya wazi ya Wimbledon itayofanyika mwezi ujao.