Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham ajiunga na Swansea kwa mkopo

Tammy Abraham is understood to have a future at Stamford Bridge, which is why Chelsea want only to loan him out Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tammy Abraham

Klabu ya Swansea City imekubali kumasajili mshambuliaji Tammy Abraham kwa mkopo kutoka Chelsea kwa msimu wa 2017-2018.

Swansea wamekabili upinzani kutoka kwa Newcastle na Brighton kwa mshambuliaji huyo wa miaka 19 ambaye alifunga mabao 23 katika mechi 40 akiwa kwenye mkopo na klabu ya Bristol City msimu wa 2016-2017.

Man City haina nia ya kumuuza Sergio Aguero

Mpango huo unatarajiwa kukamilika leo.

Abraham alifanya kazi na Paul Clement wakati meneja huyo wa Swansea alikuwa kocha huko Stamford Bridge.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tammy Abraham alifunga mabao 23 katika mechi 40 akiwa kwenye mkopo na klabu ya Bristol City