Urusi yalala kwa Ureno, New Zealand yatupwa nje kombe la mabara

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Ureno wakishangilia goli lilifungwa na Cristiano Ronaldo

Wenyeji wa michuano ya kombe la mabara timu ya taifa ya Urusi wamepoteza mchezo wao wa pili dhidi ya timu ya taifa ya Ureno kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa katika dimba la Spartak Jijini Moscow.

Mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo ndie aliyefunga goli pekee katika mchezo huo katika dakika ya nane ya mchezo akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa kutoka upande wa kushoto na Raphael Guerreiro.

conf Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mfungaji wa goli la kwanza la Mexico Raul Jimenez

Katika mchezo wa pili wa michuano hiyo Mexico waliwachapa vibonde New Zealand kwa mabao 2-1 na kuwaondosha mashindanoni .

Mabao ya Mexico yakifungwa na Raul Jimenez na Oribe Peralta huku goli pekee la New Zealand likifungwa na mshambuliaji wake Chris Wood.

kwa Matokeo ya michezo hiyo Mexico wanaongoza kundi A wakiwa na alama 4, Ureno wako katika nafasi ya pili kwa alama 4 wenyeji Urusi wana alama 3 katika nafasi ya tatu.