Salah kufanyiwa vipimo vya afya leo

Liverpool Haki miliki ya picha Google
Image caption Mohamed Salah

Winga wa klabu ya As Roma ya nchini Italia Mohamed, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na liverpool, kwa dau la pauni milion 34.

Mchezaji huyu raia wa Misri mwenye miaka 25 amekua akihitajika na kocha Jurgen Klopp, katika kuweza kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Dau la usajili la Salah, litakuwa sawa na la nyota mwingine wa Liverpool Sadio Mane, ambae alisajiliwa mwaka 2016 kwa dau kama hilo la pauni milion 34, huku Andy Carroll, akiendelea kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa zaidi mwaka 2011 aliposajiliwa kwa kiasi cha pauni milioni 35.

Mwaka 2014 Salah alikaribia kujiunga na majogoo hao wa Anfield akitokea Fc Basle kabla ya Chelsea kuwazidi Ujanja.

Salah alikua mchezaji muhimu wa As Roma msimu uliopita kwa kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili katika Serie A akifunga mabao 15 katika michezo 31 aliyocheza .