Stars yaenda Afrika kusini kushiriki michuano ya Cosafa

stars
Image caption Magolikipa wa timu taifa ya Tanzania Aishi Manula (Kushoto) na Benno Kakolanya

Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Tanzania 'Taifa Stars', kimeondoka kuelekea nchini Afrika Kusini kushiriki michuano Kombe la Castle Cosafa.

Taifa Stars wao wamepangwa katika kundi A na wapinzania wao katika kundi hilo ni timu za Mauritius, Malawi na Angola.

Katika kundi B kuna timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar pamoja na Zimbabwe, michuano hiyo itaanza kutimua vumbu kuanzia Juni 25.

Mwenyeji Afrika ya kusini,Botswana, Zambia, Namibia, Lesotho na Swaziland watacheza michezo maalumu za mchujo (play off) kuwania kuingia robo fainali.