Hamilton amlaumu Vettel kwa kumvurugia ushindi

Madereva hawa wawili wamekuwa na upinzani mkali kwa muda mrefu
Image caption Madereva hawa wawili wamekuwa na upinzani mkali kwa muda mrefu

Dereva Lewis Hamilton amesema kitendo cha dereva mwenzake Sebastian Vettel kumgonga wakati wa mbio za Azerbaijan Grand Prix ni cha aibu na hakipaswi kufanywa na dereva makini.

Madereva hao wawili waligongana wakati mbio hizo zikikaribia mwisho baada ya Vettel kuvamia nyuma ya gari la Hamilton na kisha wote wawili kupoteza muelekeo.

Image caption namna magari hayo yalivyogongana

Vetel anasema Hamilton alishika breki kwa maksudi ili kumjaribu.

Hamilton akapinga hilo na kusema kitendo hicho sio cha kimichezo.