Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 26.06.2017 na Salim Kikeke

Harry Kane Haki miliki ya picha Getty Images

Maduka ya kamari yameweka dau la kuashiria kuna uwezekano mkubwa wa Harry ane kuondoka Tottenham na kwenda Manchester United (Daily Star).

Hata hivyo Tottenham wametupilia mbali uwezekano wa Harry Kane kwenda Old Trafford na kusema thamani ya mshambuliaji wao ni karibu pauni milioni 200 (Independent).

Alex Sandro, 26, amekubali kujiunga na Chelsea huku mabingwa hao wa England wakikaribia kukamilisha mkataba wa pauni milioni 61 kumsajili beki huyo wa Juventus (Corriere della Sera).

Sandro huenda akaungana na Virgil van Dijk, 25, kutoka Southampton, na mshambuliaji Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton na kiungo mkabaji wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, wakati Chelsea ikijiandaa kutumia pauni milioni 240 msimu huu (Daily Express).

Arsenal na Manchester City wanafikiria kubadilishana washambuliaji, Alexis Sanchez, 28, kwa Sergio Aguero, 29 (Daily Star).

Hata hivyo Alexis Sanchez ameshawishiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa, Arturo Vidal, kwa kuambiwa aachane na Arsenal na kwenda katika "klabu bora duniani" Bayern Munich (Sun).

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, amewasiliana na rais wa Lyon, kabla ya kufanikisha uhamisho wake kwenda Ufaransa msimu huu (Independent).

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Arturo Vidal alitoka Juventus kabla ya kujiunga na Bayern Munich

Dau la Everton la Pauni milioni 30, la kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, limekataliwa (Mirror).

Chelsea huenda wakapanda dau la pauni milioni 35 kumtaka beki wa Roma Kostas Manola, 26, ambaye inasemekana alikuwa anakaribia kuhamia Zenith St Petersburg ya Urusi (Express).

Meneja wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson amemhakikishia mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, 31, kuwa atapata 'uzoefu mzuri' iwapo ataamua kwenda kucheza ligi ya China (Daily Mail).

Renato Sanches, 19, anayenyatiwa na Manchester United amejiweka mbali na taarifa zinazomhusisha na kuhamia Old Trafford na kusema anatarajia kubakia Bayern Munich (Record).

Juventus watapanda dau la pauni milioni 15 kumtaka beki wa kulia wa Southampton Cedric Soares (Sun).

Mshambuliaji Kylian Mbappe, 19, atapewa ongezeko la mshahara la asilimia 900 na klabu yake ya Monaco ili kumzuia asiende Real Madrid au Arsenal au Liverpool zinazomtaka (Sun).

Rais wa Real Madrid Florentino Perez alikutana na familia ya Kylian Mbappe mapema mwezi huu (Telefoot).

Arsenal na Barcelona zinapigania kutaka kumsajili kinda wa Braga, Pedro Neto, 17, ambaye huenda akawa mchezaji wa miaka 17 aghali zaidi katika historia ya kandanda, nyuma tu ya Alexandre Pato. Tayari Braga wamekataa dau la Arsenal la pauni milioni 13.2 (A Bola).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sanches alichezea Ureno mechi sita katika Euro 2016 na kufunga bao moja

Mshambuliaji wa AC Milan M'Baye Niang ana matumaini kuwa Arsenal watapanda dau la kumtaka, baada ya kuchelewesha uhamisho wake wa kwenda Everton (Calciomercato.com).

Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Radja Nainggolan kutoka Roma (Il Tempo).

Liverpool wanamfuatilia Max Meyer, 21, anayeichezea timu ya taifa ya Ujerumani chini ya miaka 21 kwenye michuano inayoendelea nchini Poland, lakini wanakabiliwa na ushindani pia kutoka Tottenham kumsajili kiungo huyo wa Schalke (Daily Star).

Crystal palace watamuulizia mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20, ambaye pia anasakwa na West ham, na Leicester (Mirror).

RB Leipzig hawana mpango wa kumuuza Naby Keita kwa bei yoyote chini ya euro milioni 80. Liverpool wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Guinea (Bild).

Liverpool wamekataa mkataba wa kubadilishana Faozi Ghoulam kutoka Napoli kwenda Anfield na Alberto Moreno kwenda Italy (Liverpool Echo).

Kiungo mchezeshaji wa Real Madrid James Rodriguez bado anataka kuhamia Manchester United baada ya kukubaliana maslahi binafsi na Old Trafford (Diario Gol).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption James Rodriguez

Manchester United huenda wakamfuata winga wa Fiorentina Federico Bernardeshi iwapo watashindwa kumsajili Ivan Perisic (Football Italia).

Borussia Monchengladbach wanataka kumchukua mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen (Sunday people).

Barcelona huenda wakamgeukia kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez iwapo watashindwa kumpata Marco Verratti (AS).

Meneja mpya wa Barcelona Ernesto Valverde anataka kupiga hatua ya kushangaza ya kumtaka kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic (Don Balon).

Bournemouth wanakaribia kukamilisha mkataba wa kudumu wa pauni milioni 20 kumsajili beki wa Chelsea Nathan Ake (The Sun).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nathan Ake

Na hatimaye….

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang alifunga magoli sita akicheza na baba yake timu moja katika mechi ya kirafiki dhidi ya maveterani wa Paris FC (tovuti ya Paris FC)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Eid Mubarak!!!! Na Jumatatu njema.

Mada zinazohusiana