Madai ya Ufisadi ya Qatar 2022 yachapishwa Ujerumani

Ripoti hiyo ya Bild inashirikisha maelezo ya kitita cha $2m kilicholipwa mtoto wa miaka 10 wa afisa mmoja wa Fifa. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ripoti hiyo ya Bild inashirikisha maelezo ya kitita cha $2m kilicholipwa mtoto wa miaka 10 wa afisa mmoja wa Fifa.

Madai ya ufisadi katika mafanikio ya Qatar kuandaa kombe la dunia la 2022 yamechapishwa katika vyombo vya habari nchini Ujerumani.

Gazeti la The Bild linasema kuwa ripoti hiyo ya 2014 ''iliokandamizwa'' iliandaliwa na aliyekuwa afisa huru wa maadili katika shirikisho la soka duniani Michael Garcia.

Ripoti hiyo ya Bild inashirikisha maelezo ya kitita cha $2m kilicholipwa mtoto wa miaka 10 wa afisa mmoja wa Fifa.

Garcia alijiuzulu mwezi Disemba 2014 akipinga vile ripoti yake ilivyochukuliwa kuhusu zabuni za kuandaa michezo hiyo.

Wakili huyo wa Marekani alishutumu ukosefu wa uongozi bora katika shirikisho hilo wakati alipoondoka, huku viongozi hao wakichapisha ripoti nyengine kama hiyo ambayo iliiondolea makosa yoyote ya ufisadi Qatar.

Gazeti hilo la Bild limesema kuwa litakuwa likichapisha maelezo ya ripoti hiyo ya Garcia yenye kurasa 403 kuanzia Jumanne ijayo.