''Serena Williams angeorodheshwa wa 700 iwapo angecheza tenisi ya wanaume''

''Serena Williams angeorodheshwa wa 700 iwapo angecheza tenisi ya wanaume'' Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption ''Serena Williams angeorodheshwa wa 700 iwapo angecheza tenisi ya wanaume''

Serena Williams angeshindwa kuwa katika nafasi ya 700 iwapo angeshiriki katika tenisi ya wanaume kulingana na bingwa mara saba wa taji la Grand Slam John Mc Enroe.

Na mchezaji anayeorodheshwa katika nafasi ya 701 duniani- Dmitry Tursunov anaamini anaweza kumshinda Serena.

Akizungumza na kituo cha habari cha NPR, Mc Enroe alizungumza kuhusu bingwa huyo wa tenisi upande wa wanawake Serena Williams ambaye ameshinda rekodi ya mataji 23 ya Grand Slam: Iwapo angecheza katika tenisi ya wanaume angekuwa nafasi ya 700 duniani.

Alifanikisha matamhsi yake kwa kusema: Hiyo hainaamishi kwamba Serena sio mchezaji mzuri na kwamba chochote kinawezekana, pengine mchezaji wa kike wa tenisi anaweza kuwa bora zaidi ya yeyote.

Lakini aliongezea: Sijaona hilo katika mchezo huo na pia sijaona katika tenisi.

Iwapo angeshiriki katika tenisi ya wanaume ingekuwa habari nyengine tofauti kabisa.

Williams baadaye alijibu katika Twitter: Ndugu John nakuenzi na nakuheshimu lakini tafadhali tafadhali usiniweke katika matamshi yako ambayo hayana msingi wowote.

Sijawahi kucheza dhidi ya mtu yeyote huko na wala sina mda wa kufanya hivyo.

Niheshimu mimi na haki yangu ya faragha nikijaribu kupata mtoto.Siku njema.