Everton wamnunua mchezaji wa Nigeria

Henry Onyekuru (kulia) alifunga mabao 22 katika klabu ya Eupen msimu uliopita Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Henry Onyekuru (kulia) alifunga mabao 22 katika klabu ya Eupen msimu uliopita

Everton wanakaribia kumnunua mshambuliaji chipukizi wa Nigeria anayevuma sana Henry Onyekuru kutoka klabu ya KAS Eupen ya Ubelgiji.

Wanatarajwia kumnunua mchezaji huyo kwa £7m.

Onyekuru, 20, alifunga mabao 22 katika klabu hiyo inayocheza ligi kuu ya Ubelgiji msimu uliopita.

Alikuwa amehusishwa na kuhamia Arsenal, West Ham United na klabu nyingine kadha Ulaya zilikuwa pia zinamtaka.

Hata hivyo, mchezaji huyo, inaarifiwa tayari alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu Everton siku ya Jumatatu.

Onyekuru anatarajiwa kutumwa Anderlecht kwa mkopo mwaka mmoja, aendelee kuimarika akicheza soka Ubelgiji.

Anachukuliwa na mkurugenzi wa soka wa Everton Steve Walsh pamoja na meneja Ronald Koeman kuwa mchezaji atakayewafaa sana siku za usoni.

Onyekuru alichezea timu ya taifa ya Nigeria mara yake ya kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Togo mapema mwezi huu ambayo walishinda 3-0.

Mada zinazohusiana