Je unamfahamu mcheza soka mstaafu raia wa Senegal Salif Diao?

Salif Diao
Image caption Salif Diao

Salif Diao aliondoka nyumbani kwao huko K├ędougou, kusini mwa Senegal akiwa na umiri wa miaka 13 kufuata ndoto yake ya kuwa mcheza soka wa kulipwa.

Safari yake ilimpeleka hadi mjini Dakar mji mkuu wa Senegal, ambapo wakati mwingine alilala nje ya uwanaj wa kitaifa na kuwaoshea saharni walinzi wa uwanja ili angalau aweze kupata chakula.

Ilikuwa sehemu ya safari iliyompleka hadi Liverpool, moja ya vilabu vikubwa zaidi duniani.

Image caption Baada ya miaka 17 kama mchezaji wa kulipwa, Seif Dialo sasa amestaafu na kurudi tena nyumbani alikoanzia.

Baada ya miaka 17 kama mchezaji wa kulipwa, Seif Dialo sasa amestaafu na kurudi tena nyumbani alikoanzia.

Kuitafuta ndoto yake hiyo, ina maana kuwa angeacha kusoma. Akiiangalia taaluma ambayo imempa pesa na umaarufu, kile tu anachojutia ni kuwa aliwacha masomo na kuenda kucheza soka ya kulipwa.

"Imekuwa safari ngumu kuanzia nikitoka nyumbani nikiwa umri wa miak 13, na hadi wakati nikiikamisliha taaluma yangu," alisema Diao.

Image caption Baada ya miaka 17 kama mchezaji wa kulipwa, Seif Dialo sasa amestaafu na kurudi tena nyumbani alikoanzia.

Diao hakuweza kutimiza malengo yake ya elimu kwa sababu ya mahitaji yanayotokana na taaluma ya soka ya kulipwa.

Kutokana na hilo, Diao alianzisha wakfu wa Salif Diao Foundation miaka mitatu iliyopiya. Wakfu huu una lengo la kuwakuza wachezaji walio na kisomo.

Licha ya soka kumpa maisha mazuri, anahisi kuwa njia pekee ambayo ataishukuru jamii ni kuwashauri wacheza soka wachanga kuwa na kitu cha kuwasaidia nyakati ngumu.

Image caption Baada ya miaka 17 kama mchezaji wa kulipwa, Seif Dialo sasa amestaafu na kurudi tena nyumbani alikoanzia.

Mada zinazohusiana