Uingereza yatupwa nje michuano ya Ulaya U21

Uingereza ilikua na matumaini ya kunyakua kikombe hicho kama walivyofanya wachezaji wa miaka chini ya 18 siku chache zilizopita waliobeka kombe la dunia
Image caption Uingereza ilikua na matumaini ya kunyakua kikombe hicho kama walivyofanya wachezaji wa miaka chini ya 18 siku chache zilizopita waliobeka kombe la dunia

Timu ya vijana wa miaka chini ya 21 ya Uingereza imekosa nafasi ya kufuzu hatua ya fainali michuano ya bara la Ulaya baada ya kupoteza kwa penalti 4-3 mbele ya Ujerumani.

Awali Uingereza ilitangulia kupata goli kwa Demarai Gray dakika ya 41 kabla Ujerumani kusawazisha kupitia Davie Selke dakika ya 35.

Kipindi cha pili Uingereza ilianza kwa kasi tena na kupata goli la pili lililofungwa na Tammy Abraham mnamo dakika ya 50 ambalo pia lilisawazishwa na Felix Platte dakika ya 70.

Ujerumani kwa sasa itakipiga na Uhispania ambao waliwachapa Italia 3-1 siku ya Ijumaa.