Chile: Tutamkaba Ronaldo asipate mipira nusu fainali

Cristiano Ronaldo
Image caption Cristiano Ronaldo

Chile itajaribu kuzuia mipira kutomfikia nyota wa timu ya Ureno Cristiano Ronaldo wakati mataifa hayo mawili yatakapokutana katika kipute cha nusu fainali cha kombe la Confederation mjini Kazan kulingana na Midfielder Marcelo Diaz.

Mshambuliaji wa Real Madrid Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 alifunga mara mbili kuisaidia nchi yake kufika katika awamu hiyo nchiniu Urusi.

Sote tunajua kuwa ni mchezaji mzuri, ni hatari sana na anaweza kubadilisha mechi akiwa pekee.

Amekuwa na msimu mzuri.Anacheza hapa na nguvu zilezile.

Hatma ya Ronaldo baada ya soka haijulikani huku kukiwa na ripoti kwamba anataka kuondoka Real Madrid baada ya kushutumiwa kukwepa kulipa ushuru na mamlaka za Uhaispania.

Lakini yuko katika hali nzuri uwanjani baada ya kufunga mara 16 katika mechi 10 zilizopita kwa klabu na taifa.

''Swala muhimu hapa ni kumzuia kupata mipira'', alisema Diaz.

Mkufunzi wa Ureno Fernando Santos atachunguza hali ya kiungo mpya wa Manchester City Bernado Silva ambaye alihisi uchungu mwingi katika mguu wake wa kulia baada ya kufunga katika mechi ya ushindi siku ya Jumamosi dhidi ya New Zealand