Tyson Fury ataka kuzipiga na Anthony Joshua nchini Nigeria

Anthony Joshua baada ya ushindi wake wa Knockout dhidi ya Wladmir Klitschko Haki miliki ya picha PA
Image caption Anthony Joshua baada ya ushindi wake wa Knockout dhidi ya Wladmir Klitschko

Bondia wa Uingereza katika uzani mzito duniani Tyson Fury anataka kuzipiga na Anthony Joshua ambaye ana mizizi ya Nigeria katika mji mkuu wa Nigeria Lagos.

Katika kanda ya video iliochapishwa katika mtandao wa You Tube ,Fury anasema kwamba yeye ndio 'njozi mbaya' ya Anthony Joshua.

Alikuwa tayari amekubali kupigana na Joshua baada ya ushindi wake dhidi ya Wladmir Klitschko.

Joshua ambaye alimpiga knockout raia huyo wa Ukrain katika raundi ya 11 katika uwanja wa Wembley baada ya pigano hilo alimtaka Tyson Fury abaye pia alimshinda Klitschko katika pigano jingine.

Image caption Bondia wa Uingereza Tyson Fury

''Fury uko wapi'', aliuliza..''najua amekuwa akizungumza sana, ningependa kuwapatia mashabiki wetu 90,000 fursa ya kutuona''.

Fury ambaye hajapigana tangu alipomshinda Klitschko alijibu ''tucheze''.