Ujerumani yaichapa Mexico 4-1 kombe la mabara

Leon Goretzka anahusishwa kujiunga na Arsenal msimu ujao
Image caption Leon Goretzka anahusishwa kujiunga na Arsenal msimu ujao

Ujerumani imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya kuichapa bila huruma Mexico 4-1.

Leon Goretzka alifunga mara mbili katika mtanange huo katika dakika ya 6 na 8.

Magoli mengine ya Ujerumani yaliwekwa kimiani na Timo Werner dakika ya 59 na Amin Younes dakika ya 90.

Image caption Ujerumani walitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa

Goli la kufutia machozi kwa upande wa Mexico lilipachikwa na Marco Fabian dakika ya 89.

Mexico walipata nafasi nyingi lakini hawakuweza kuzitumia vyema huku Ujerumani ikionekana kukomaa vilivyo katika safu ya ulinzi.

Image caption Iliwachukua Mexico dakika 89 kuweza kumfunga Marc-Andre ter Stegen

Fainali ya kombe la mabara itapigwa jumapili ya Julai 2 mbili kati ya Ujerumani na Chile mjini St Petersburg, huku mchezo wa awali ukizikutanisha Ureno na Mexico kutafuta mshindi wa tatu.