Venus Wiliams ahusika katika ajali mbaya ya barabarani

Nyota wa mchezo wa tenisi Venus Williams amehusika katika ajali mbaya ya barabarani iliomuua mwanamume wa miaka 78. Haki miliki ya picha Press Association
Image caption Nyota wa mchezo wa tenisi Venus Williams amehusika katika ajali mbaya ya barabarani iliomuua mwanamume wa miaka 78.

Nyota wa mchezo wa tenisi Venus Williams amehusika katika ajali mbaya ya barabarani iliomuua mwanamume wa miaka 78.

Msemaji wa kituo cha polisi cha Palm Beach Gardens mjini Florida aliithibitishia BBC kwamba walikuwa wanachunguza ajali hiyo iliomuhusisha bingwa huyo wa taji la Grand Slam.

Mtu mmoja alipelekwa hospitali baada ya ajali hiyo iliofanyika tarehe 9 mwezi Juni na kufariki wiki mbili baadaye kutokana na majeraha ,alisema.

Kulingana na chombo cha habari cha TMZ, ambacho kilitoa habari hiyo, maafisa wa polisi wanaamini kwamba Williams ni wa kulaumiwa lakini wakili wake anasema kuwa ilikuwa ajali.

Mtu aliyefariki ,Jerome Barson, alikuwa akisafiri na mkewe aliyekuwa akiendesha gari hilo kupitia eneo la makutano wakati ajali hiyo ilipotokea.

''Gari la bi Williams lilingia kwa haraka katika barabara yao halikuweza kuondoka kwa haraka kutokana na msongamano wa magari barabarani kulingana na taarifa ya shahidi katika ripoti ya polisi iliopatikana na vyonbo vya habari.

Bi Barson pia alipelekwa hospitalini lakini akapona.

Bi Williams ana makosa kwa kukiuka sheria ya kumpatia heshima dereva aliye na haki ya kupita, ripoti hiyo ilisema, ikiongezea kwamba hakukuwa na maswala mengine kama vile ushawishi wa dawa za kulevya, pombe ama hata kusumbuliwa na simu ya rununu.