Manny Pacquiao apigwa na mwalimu wa zamani

Jeff Horn celebrates winning the world title Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeff Horn

Mwalimu wa zamani wa shule nchini Australia Jeff Horn ameshangaza ulimwengu wa ndondi kwa kumshinda bingwa wa dunia raia wa Ufilipino Manny Pacquiao wa ufilipino .

Jeff Horn alishinda kwa pointi katika pambano la raundi kumi na mbili na kupata taji la welterweight mbele ya mshabiki elfu hamsini.

Kabla ya pambano hilo kuanza watazamaji wengi walidhani kuwa Horn mwenye umri wa miaka ishirini na tisa hakuwa na matumaini yoyote ya kukabiliana vilivyo na Manny.

Kushindwa kwa Manny Pacquiao kumewashangaza mashabiki wengi nchini ufilipino ambako yeye ni nyota wa kitaifa na seneta aliyechaguliwa.

Pacquiao ambaye ana umri wa thelathini na nane ni mmojawapo wa wanamasumbwi mashuhuri wa kizazi cha sasa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Manny Pacquiao (kulia)