Stars yaichapa Afrika Kusini kwao

COSAFA Haki miliki ya picha Google
Image caption Mshambuliaji wa Tanzania Elias Maguri akichuana na mchezaji wa Afrika Kusini

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wameichapa timu ya Taifa ya Afrika kusini kwa bao 1-0 katika michuano ya kombe la Cosafa.

Bao la dakika ya 18 la mshambuliaji Elias Maguri lilitosha kuipeleka Stars katika nusu fainali ya michuano katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Royal Bafokeng, Rusternburg.

Tanzania sasa itamenyana na Zambia siku ya Jumatano katika mchezo wa nusu fainali, wakati Afrika Kusini wanaangukia kwenye michuano ya Plate, inayoshirikisha timu zilizotolewa hatua ya robo fainali.

Katika mchezo wa pili wa michuano hiyo Zimbabwe waliwachapa Swaziland kwa mabao 2-1.