Michuano ya tenesi ya Wimbledon kuanza leo

Wimbledon Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Andy Murray bingwa mtetezi wa michuano ya Wimbledon

Michuano ya tenesi ya Wimbledon itaaanza leo nchini England kwa nyota wa mchezo huo kuwania taji la michuano hiyo na itafikia tamati julai 16.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo Mwingereza Andy Murray , ataanza kutupa karata yake dhidi ya Alexander Bublik kutoka Kazakhstan.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo kwa upande wa wanawake Serena Williams hatoshiriki kwa kuwa anasubiri kujifungua.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Johanna Konta

Mchezaji namba moja wa Uingereza kwa upande wa wanawake Johanna Konta atashuka dimbani kuchuana na Su-Wei Hsieh. Venus Williams, yeye ataanza na Elise Mertens.

Nyota wengine watakaoshuka dimbani ni Jo-Wilfried Tsonga atacheza na Cameron Norrie, Rafael Nadal atakua na kibarua mbele ya John Millman. Joao Sousa atacheza na Dustin Brown