Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 03.07.2017 na Salim Kikeke

Neymar Haki miliki ya picha Reuters

Manchester United na Paris St-Germain wako tayari kutoa £174m kumfungua mshambuliaji wa Barcelona Neymar kutoka kwa mkataba wake katika klabu hiyo iwapo mchezaji huyo ataamua kuihama klabu hiyo ya Uhispania (Don Balon kupitia Daily Star).

Arsenal wanakaribia kutangaza usajili wa winga kutoka Algeria, Riyad Mahrez, 26 ambaye anaichezea Leicester City (Calciomercato).

Paris Saint Germain wamemuulizia kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, huku Liverpool wakisema mchezaji huyo kutoka Brazil ana thamani ya pauni milioni 87 (Daily Mirror).

Chelsea wana matumaini wataweza kufanikisha mpango wa kumsajili beki wa kushoto kutoka Brazil, Alex Sandro, 26, huku mazungumzo na Juventus yakitarajiwa kufanyika Jumatatu (Daily Telegraph).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alwex Sandro alichezea Juventus fainali ya Uefa mjini Cardiff ambapo walichapwa na Real Madrid

Antonio Conte anakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City katika kutaka kumsajili beki wa kati wa Roma Antonio Rudiger, 24. Barcelona pia wanataka kumsajili Leonardo Bonucci, 30, ambaye Chelsea wanamtaka, na Juventus wamempa mkataba mpya Sandro ili kumsawishi asiondoke (Daily Mirror).

Jurgen Klopp ameiambia Liverpool kuongeza bidii katika kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, ambaye atakuwa na mazungumzo na klabu yake kuhusu mustakbali wake nchini Ujerumani (Times).

Nahodha wa zamani wa England na Chelsea John Terry, 36, anatazamiwa kuthibitishwa kuwa mchezaji wa Aston Villa siku ya Jumatatu (Daily Telegraph).

Kocha mkuu wa Monaco Leonardo Jardim ana matumaini kuwa Kylian Mbappe, 18, hataondoka, lakini amekiri kuwa wachezaji wengi huenda wakaondoka msimu huu (RMC).

Tottenham wamepanda dau kwa mara ya pili la pauni milioni 27 kumtaka kiungo wa Sporting Lisbon Adrien Silva, 28, (A Bola).

Chelsea wamemuulizia beki wa Real Madrid Danilo, 25 (Marca).

Beki wa Paris St-Germain anayenyatiwa na Manchester City, Marquinhos, 23, amesaini mkataba mpya wa mude mrefu kubakia Ufaransa (Independent).

Newcastle wanafikiria kumchukua beki wa Arsenal Kieran Gibbs (Daily Mirror).

Haki miliki ya picha Getty Images

Paris Saint-Germain wamemuulizia kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, huku Barcelona pia wakimnyatia mchezaji jhuyo kutoka Brazil (Daily Mirror).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Tetesi kuhusu wachezaji Ulaya

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumatatu njema.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii