Everton yakamilisha usajili wa Keane

everton Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michael Keane baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Everton

Klabu ya Everton imekamilisha usajili wa beki wa kati Michael Keane kutoka Burnley, kwa dau litalofikia pauni milioni 30 na kuweka rekodi ya klabu hiyo.

Keane amesaini mkataba wa miaka mitano kuichezea klabu hiyo na unakua usajili wa tano kwa Everton katika majira kiangazi.

Everton tayari imewasajili golikipa Jordan Pickford, kiungo Davy Klaasen, mshambuliaji Sandro Ramirez pamoja na Henry Onyekuru.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji mpya wa Everton Sandro Ramirez

The toffes imekwisha tumia kiasi cha pauni milioni 96 katika usajili wa nyota hao wapya .

Klabu ya zamani ya Michael Keane, Man United itapata mgawo wa kiasi cha pauni milioni 7.5 katika usajili huo.