Murray, Nadal waanza kwa ushindi

Wimbledon Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Andy Murray

Nyota wa mchezo wa tenesi Andy Murray na Rafael Nadal wameanza vyema michuano ya tenesi ya Wimbledon.

Murray alimshinda mpinzani wake Alexander Bublik kwa seti tatu kwa 6-1 6-4 na 6-2.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rafael Nadal

Nae Rafael Nadal akashinda kwa seti tatu dhidi ya John Millman kwa 6-1 6-3 na seti ya mwisho akashinda kwa 6-2.

Mfaransa Jo-Wilfried Tsonga alimchapa Cameron kwa seti tatu, huku Mjapani Kei Nishikori akishinda kwa seti tatu dhidi ya Marco Cecchinato