Mwanawe George Weah ajiunga na PSG

Timothy Weah ajiunga na PSG
Maelezo ya picha,

Timothy Weah ajiunga na PSG

Tomothy Weah amefuata nyayo za babake ambaye ni mshindi wa taji la Ballon d'Or George Weah baada ya kutia saini kandarasi na klabu ya Paris St- Germain.

Mshambuliaji huyo wa miaka 17 ametia saini mkataba wa miaka 3 na PSG klabu ambayo George Weah aliiwakilisha kutoka mwaka 1992 hadi 1995.

Tayari kumekuwa na uvumi kwamba mwana anafuata nyayo za babake.

Mnamo mwezi Septemba 2016, kinda Weah alifunga hat-trick katika ushindi wa 8-1 dhidi ya klabu ya Ludogorets katika mechi yake ya kwanza ya Uefa.

''Ni fahari kubwa kuendeleza pale baba alipowachia'' , alisema Weah ambaye alizaliwa mjini New York na kujiunga na New York Red Bulls kabla ya kujiunga na chuo cha mafunzo ya soka cha PSG mnamo mwezi Julai 2014.

''Niko katika klabu kubwa na natumai nitaendelea kuimarika ili niweze kuichezea timu kubwa''.

Maelezo ya picha,

George Weah wakati alipokuwa akiichezea PSG

Babake mwenye umri wa miaka 50 kutoka Liberia aliwahi kushinda mara tatu taji la mwanasoka bora wa Afrika na mchezaji wa pekee wa Afrika kuwahi kushinda taji la Ballon d'Or mwaka 1995.

Alijipatia umaarufu katika klabu ya Monaco 1988 na kufanikiwa kuzichezea PSG na AC Milan muongo uliofuata.

Pia aliichezea Chelsea na Manchester City katika ligi ya Uingereza katika miaka ya mwisho ya soka yake.