Mourinho :Sifurahishwi na usajili

Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amedaiwa kutofurahishwa na taratibu za usajili zinavyoendelea wa kipindi hiki cha majira ya kiangazi katika klabu yake .

Baada ya United kutwaa taji la michuano ya Europa ligi,meneja huyo alisema alimpa makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward orodha na wachezaji anaowahitaji kusajili.

Man United haijafanikiwa kusajili wachezaji ambao kocha huyu anawataka katika kujenga kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao.

Kuna uwezekano kukawa na maendeleo mengine wiki hii lakini mpaka sasa ni mchezaji mmoja mpya aliyesajili ambaye ni beki Victor Lindelof toka Benfica ya Ureno.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Victor lindelof

Mourinho anahitaji mshambuliaji mmoja atakayeziba pengo la Zlatan Ibrahimovic, pamoja na kiungo mkabaji.

Man United wamekuwa wakimuwania mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata ambae uhamisho wake bado haujulikani hatima yake.

Lakini pia timu hiyo inawahitaji viungo Eric Dier wa Tottenham na Nemanja Matic kuja kujenga safu bora ya kiungo cha chini .