Besiktas yamnasa kisiki Pepe

Pepe Haki miliki ya picha Besiktas twitter
Image caption Pepe akitambulishwa baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu

Klabu ya Besiktas ya Uturuki imefanikiwa kumsajili bure beki kisiki wa timu ya taifa ya Ureno, Képler Laveran Lima Ferreira, maarufu kama Pepe.

Pepe amesaini mkataba wa miaka wa mitatu kuweza kuwatumikia miamba hao wa ligi ya Uturuki.

Mchezaji huyu aliachwa na klabu yake ya Real Madrid baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa msimu uliopita.

Image caption Pepe alitajwa mchezaji bora katika fainali za Euro 2016

Uhamisho huu wa mlinzi huyu unahitimisha miaka kumi ya kuitumikia Real Madrid ambapo alikua ni moja kati ya wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza wa timu hiyo.