Lille kuwatema wachezaji 11 wakiwemo Enyama, Sunzu

LILLE Haki miliki ya picha Google
Image caption Vicenti Enyama

Golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Vincenti Enyama, ni moja kati ya wachezaji kumi na moja walioambiwa na kocha wa Lille,Marcelo Bielsa, hawahitajiki katika klabu hiyo msimu ujao.

Enyama ambae aliichezea timu ya taifa ya Nigeria michezo 101 alisaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu msimu uliopita

Bielsa ambae ni kocha mpya katika timu hiyo pia amewatumia ujumbe mchezaji Stoppila Sunzu,raia wa Zambia, Mtunisia Naim Sliti na Junior Tallo kutoka Ivory Coast kuwataarifu hawako katika mipango yake.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Stoppila Sunzu

Lille tayari imemsajili golikipa wa kimataifa wa Burkina Herve Koffi, mabadiliko haya yanakuja baada ya timu hiyo kumaliza katika anfasi ya kumi na moja msimu uliopita