Lacazette afanyiwa ukaguzi wa kimatibabu Arsenal

Lacazette afanyiwa vipimo vya matibabu Arsenal Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lacazette afanyiwa vipimo vya matibabu Arsenal

Mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette amekamilisha ukaguzi wa kimatibabu kabla ya kujiunga na Arsenal kwa kitita cha rekodi ya pauni milioni 45.

The Gunners ilikuwa imetoa kitita cha chini lakini kikakataliwa na hivyobasi kuendelea na mazungumzo.

Kitita hicho cha hadi pauni milioni 52 kitapita kile alichonunuliwa Mesut Ozil kutoka Real Madrid cha pauni milioni 42.4 2013.

Lazazette alikuwa wa pili kwa idadi ya mabao katika ligue ! Msimu uliopita akiwa na mabao 28.

Amefunga mabao 129 katika mechi 275 katika mashindano yote tangu alipoanza kuchezeshwa katika timu kikosi cha kwanza 2009-10.

Alishinda kwa mabao na mshambuliaji wa PSG Edison Cavani aliyefunga mbao 35.

Lacazzette ambaye ameichezea Ufaransa mara 11 amehusishwa na vilabu kadhaa vikuu na alitarajiwa kujiunga na Atletico Madrid.

Wiki iliopita mkurugenzi mkuu wa Arsenal Iva Gazidis aliahidi kuwasajili wachezaji wa kiwango cha juu wakati wa mahojiano na wanahabari.

Arsenal kufikia sasa imemsajili beki wa kushoto Sead Kolasinac, ambaye alijiunga na klabu hiyo kutoka Schalke.