Messi kusalia Barcelona hadi 2021

Lionel Messi Barcelona Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lionel Messi alifunga ndoa mwishoni mwa wiki

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amekubali kutia saini mkataba mpya ambao utamuweka katika klabu hiyo hadi 2021.

Messi, 30, alijiunga na klabu ya Barca akiwa na miaka 13.

Mchezaji huyo anatarajiwa kutia saini mkataba huo atakaporejea kushiriki mazoezi.

Messi alifunga ndoa mwishoni mwa wiki mjini Rosario, Argentina.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii