Gael Clichy kujiunga na klabu ya Adebayor nchini Uturuki

Gael Clichy na Pep Guardiola Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gael Clichy aliachiliwa aondoke na Pep Guardiola

Beki wa kushoto wa zamani wa Manchester City Gael Clichy atajiunga na klabu ya Uturuki ya Istanbul Basaksehir.

Mchezaji huyo wa miaka 31 hakupewa mkataba mpya Etihad baada ya mkatana wake kumalizika mwisho wa msimu wa 2016-17.

Klabu hiyo imethibitisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla yake kutia saini mkataba Ijumaa.

Clichy alijiunga na City kutoka Arsenal mwaka 2011, na alishinda mataji ya Ligi ya Premia mara mbili na kombe moja la EFL akiwa na klabu hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu kuhamia kwake Uturuki hayajatolewa lakini taarifa Uturuki zinasema huenda beki huyo atalipwa euro 3m (£2.6m) kila msimu na kwamba mkataba wake ni wa miaka mitatu.

Clichy atajiunga sana na mshambuliaji wa zamani wa City na Arsenal Emmanuel Adebayor ambaye alijiunga na Istanbul Basaksehir mwezi Januari.

Klabu hiyo ilimaliza ya pili ligi kuu ya Uturuki msimu uliopita, ambapo Adebayor aliwafungia mabao sita ligini.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea