Shabiki wa Sunderland Bradley Lowery aliyegusa nyoyo za wengi afariki

Bradley Lowery Haki miliki ya picha PA

Shabiki wa klabu ya Sunderland wa umri wa miaka sita Bradley Lowery, ambaye tatizo lake la kiafya liligusa nyoyo za wengi amefariki dunia.

Bradley alikuwa anaugua ugonjwa ambao kwa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.

Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Bradley alisherehekea siku yake ya kuzaliwa Mei akiwa na Jermain Defoe na Vito Mannone

Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.

Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kwenye mitandao ya kijamii.

"Mvulana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo.

"Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake."

Haki miliki ya picha Owen Humphreys
Image caption Mamake Bradley Gemma Lowery alikuwa awalia mesema mvulana huyo alikuwa amedhoofika sana

Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana.

Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na hangeweza kutibiwa.

Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".

Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.

Haki miliki ya picha Picha ya Familia
Image caption Bradley alitawazwa Mtoto wa Ujasiri katika tuzo za Fahari ya Kaskazini Mashariki
Haki miliki ya picha PA
Image caption Bradley aliipenda sana Sunderland AFC na alikaribishwa uwanjani Stadium of Light
Haki miliki ya picha PA
Image caption Mkusanyiko wa picha za Bradley zilizotolewa wakati wa sherehe za siku ya sita ya kuzaliwa ya Bradley mwezi Mei mwaka huu
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wa Sunderland walikuwa na bango kubwa uwanjani la kumuunga mkono Bradley wakati wa mechi yao dhidi ya Swansea mwezi Mei
Haki miliki ya picha PA
Image caption Bradley alitembea kwenye zulia jekundu wakati wa hafla ya Tuzo za Mchezaji Mashuhuri wa Mwaka wa BBC 2016
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bradley na babake Carl mechi kati ya Everton na Sunderland

Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi mwaka jana, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Bradley aliunda urafiki na Jermain Defoe

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii