Per Mertesacker: Nahodha wa Arsenal kustaafu mwaka ujao

Per Mertesacker Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Per Mertesacker aliinua Kombe la FA akiwa na Arsenal mwezi Mei

Nahodha wa Arsenal Per Mertesacker ametangaza kwamba atastaafu mwisho wa msimu wa 2017-18 na kuwa msimamizi wa akademi ya klabu hiyo.

Beki huyo alijiunga na Arsenal kutoka Werder Bremen Agosti 2011 lakini aliwachezea mechi mbili pekee msimu uliopita kutokana na majeraha.

Arsenal wametangaza kwamba ataanza kufanya kazi na akademi ya klabu hiyo kumuandaa kwa majukumu hayo ya baadaye.

"Per ni mtu wa kipekee ambaye ni mfano mwema kwa wachezaji chipukizi," meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema.

"Hufikiria sana kuhusu mechi na huwa anajitolea kusaidia wachezaji kufikia upeo wao."

Mertesacker alirejea kutoka kuuguza jeraha na akasaidia Arsenal Arsenal kulaza Chelsea uwanjani Wembley mwezi mei na kutwaa Kombe la FA.

Mertesacker, 32, alichezea Arsenal zaidi ya mechi 200.

Mada zinazohusiana