Kenya yaizaba Uganda kriketi

Timu ya kenya ya Kriketi
Image caption Timu ya kenya ya Kriketi

Timu ya Kenya ya kriketi ya wachezaji wanaume walio chini ya umri wa miaka 19 imeicharaza Uganda kwa wiketi saba na kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia mwakani nchini New Zealand.

Uganda walianza kupiga wakaondolewa wote wakiwa na mikimbio 60 kwa overs 17.1.

Kenya walinguruma kama Simba walipopata nafasi yao ya kupiga na kuwanyamazisha Waganda kwa mikimbio 61/3 kwa overs 8.3.

Imekua ni shangwe na hoi hoi kwa wachezaji hao ambao wamemuomba mkuu wa kriketi Kenya Jackie Janmohammed wale pizza leo kwa chakula chao cha mchana.

Heko pia kwa Jackie kujitahidi kuleta mashindano haya Nairobi.