Rooney anataka Everton ishinde kombe baada ya kurejea klabu hiyo

Wayne Rooney Haki miliki ya picha PA
Image caption Rooney anataka Everton ishinde kombe baada ya kurejea klabu hiyo

Wayne Rooney anasema kuwa kushinda kombe na Everton kitakuw kilele cha ufanisi baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Manchester United.

Rooney anaitaka Everton kushinda kombe lao kuu la kwanza tangu ishinde mwaka 1995 kombe la FA

"Klabu hii inastahili kushinda vikombe na tunachukua hatua kubwa kuhakikisha kuwa tumeshinda vikombe," alisema Rooney.

Everton ambayo imetumia pauni milioni 90 msimu huu katika kununua wachezaji, imekubalii kununua ardhi huko Liverpool ambapo watajenga uwanja kwa gharama ya pauni milioni 300.

Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 31 anavaa jesi nambari 10 ambayo ilikuwa ni ya Romelu Lukaku ambaye atajiunga na Manchsertes United kwa kima cha pauni milioni 75.