Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 10.07.2017 na Salim Kikeke

Gylfi Sigurdsson (kati) Haki miliki ya picha Huw Evans Agency
Image caption Gylfi Sigurdsson (kati)

Everton wametoa dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27. Wakifanikiwa watakuwa wametuia zaidi ya pauni milioni 100 za usajili msimu huu (Daily Mail).

Baada ya kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton, Manchester United huenda wakamsajili kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, baada ya kukubaliana mkataba wa pauni milioni 35. Chelsea wanamtaka pia Bakayoko (Daily Star).

Arsenal wapo tayari kupanda dau la tatu la zaidi ya pauni milioni 45 kumtaka winga wa Monaco, Thomas Lemar, baada ya dau la pauni milioni 30 na 40 kukataliwa (Daily Mirror).

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Theo Walcott alijiunga na Arsenal Januari 2006

Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 28, amedhamiria kupigania nafasi yake Emirates, licha ya kuhusishwa na kuhamia West Ham kwa pauni milioni 20 (Daily Star).

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kuimarisha eneo la kiungo kwa kumsajili Marcelo Brozovic kutoka Inter Milan (ESPN).

Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 27, ambaye amehusishwa na kuhamia Juventus, ameachwa kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Australia kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya (Sun).

Chelsea wapo tayari kutoa euro milioni 80 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata baada ya kumkosa Romelu Lukaku (AS).

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumsajili beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19 kwa pauni milioni 10 (Daily Mirror).

Real Madrid wapo tayari kumuuza kiungo Mateo Kovacic, na Tottenham wamehusishwa na kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia (Evening Standard).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wojciech Szczesny

Cristiano Ronaldo atabakia Real Madrid msimu wa 2017-18 na hivyo kufuta uvumi wa kuhamia Manchester United (AS).

Newcastle wanajaribu kukamilisha usajili wa kiungo wa Norwich Jacob Murphy, 22, kwa pauni milioni 8.5, huku Southampton na Crystal Palace wakimtaka pia mchezaji huyo (Daily Mirror).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Uingereza

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.

Mada zinazohusiana