Nadal atupwa nje michuano ya Wimbledon

Nadal alitarajia kupata taji la tatu mfululizo la Wimbledon
Image caption Nadal alitarajia kupata taji la tatu mfululizo la Wimbledon

Matumaini ya Rafael Nadal kushinda taji la tatu la Wimbledon yameyeyuka baada ya kukubali kichapo kutoka kwa Gilles Muller wa Luxembourg.

Mshindi huyo wa vikombe vikubwa 15 alianza vyema kabla ya Muller kumgeuzia kibao na kushinda kwa seti 6-3 6-4 3-6 4-6 15-13 ndani ya saa nne na dakika 47.

Image caption Muller atapambana na Marin Cilic wa Crotia katika hatua inayofuata

Kushindwa huku kumemmfanya Nadal kukosa kikombe hicho kwa mara ta tatu mfululizo kama alivyofanya kwa French Open.

Muller, 34, atapambana na Marin Cilic wa Crotia ambaye ni namba saba kwa ubora duniani katika hatua ya nane bora.