Wayne Rooney kucheza dakika 45 dhidi ya Gor Mahia Tanzania

Wayne Rooney kucheza dakika 45 dhidi ya Gor Mahia Tanzania Haki miliki ya picha Everton FC
Image caption Wayne Rooney kucheza dakika 45 dhidi ya Gor Mahia Tanzania

Mkufunzi wa klabu ya Everton Ronald Koeman yuko tayari kuiongoza klabu yake nchini Tanzania wiki hii katika mechi ya maandalizi ya msimu ujao.

The Toffees watakabiliana na klabu ya Kenya ya Gor Mahia katika uwanja wa kitaifa wa Dar es Salaam wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 siku ya Alhamisi, ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya kirafiki kabla ya msimu wa 2017/18.

Koeman amesema kuwa kila mchezaji wake akiwemo wayne Rooney atacheza dakika 45 dhidi ya Gor Mahia huku wakilenga kuimarisha viungo vyao.

Everton wako nchini Tanzania chini ya usimamizi wa wafadhili wao wapya Sportpesa, wachezaji hao pia watatembelea jamii za taifa hilo ili kuweza kujua utamaduni wa taifa hilo la Afrika mashariki.

Mpango huo utafanya ziara hiyo kuvutia zaidi na Koeman yuko tayari.

''Nimezuru mataifa kadhaa barani Afrika lakini sio Tanzania'', alisema.''Nimejiandaa vilivyo.

Huwa vigumu kucheza mechi katika eneo la mbali kutokana joto na ni lazima tucheze mechi hiyo ya kirafiki.Lakini kutokana na vile tulivyojiandaa, tutaondoka siku ya Jumanne jioni na kurudi siku ya Ijumaa.Hii ni mechi yetu ya kwanza na kila mchezaji atajumuishwa kwa dakika 45.Tunacheza mechi kushinda na tutadhihirisha hilo nchini Tanzania''.

Mada zinazohusiana