Msanii Stormzy afananishwa kimakosa na Romelu Lukaku

Stormzy kushoto na Lukaku kulia
Image caption Stormzy kushoto na Lukaku kulia

Gazeti moja la Ireland limekosea picha ya msanii Stormzy na ile ya mshambuliaji mpya wa Man United Romelu Lukaku.

Gazeti la The Herlad lilichapisha picha ya msanii huyo Stormzy likidhania ni Lukaku chini ya kichwa cha habari : Lukaku yuko tayari kufanya kazi.

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 amekamilisha uhamisho wake hadi Manchester United kwa kitita cha pauni milioni 75 baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu.

Picha za mshambuliaji huyo katika klabu yake mpya hazijatolewa, hivyobasi gazeti hilo la Ireland liliamua kutumia picha za zamani.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Hivi ndivyo gazeti la herald nchini Ireland lilivyochapisha

Tatizo ni kwamba alikuwa Stormzy ambaye ni shabiki wa Manchester United.

Stormzy ametoa maoni yake kuhusu picha hiyo ambapo hakufurahishwa.

Gazeti hilo la Herald limeomba msamaha kwa makosa hayo.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Msanii Stormzy akiwa amevalia jezi ya timu anayoshabikia ya Manchester United

Sio mara ya kwanza watu kuchanganyikiwa na picha za wawili hao ama hata kuwafananisha.

Mteja mmoja wa mtandao wa Twitter alisema kuwa ''nduguye Stormzy amejiunga na klabu ya Manchester United baada ya msanii huyo kumpongeza Rooney kwa hatua yake ya kurudi Everton