McGregor atamba kumtwanga Mayweather mzunguko wa nne

Mayweather anatajwa kuwa miongoni mwa wanamichezo wenye mvuto mkubwa duniani
Image caption Mayweather anatajwa kuwa miongoni mwa wanamichezo wenye mvuto mkubwa duniani

Bondia Conor McGregor ameahidi kumtangwa Floyd Mayweather ndani ya Round nne wawili hao walipokutana katika kulizungumzia pambano lao la Agosti 26.

Wametokea mbele ya maelfu yamashabiki wao katika mkutano na waandishi wa habari mjini Los Angeles.

Haki miliki ya picha Reauters
Image caption McGregor amesema anashangaa nini kilifanya wapiganaji wengine wakashindwa kumtwanga Mayweather

''Upinzani atakaoupata kutoka kwangu hajawahi kuupata kamwe'', alisema McGregor, 28.

Mayweather akajibu ''Nakuhakikishia nitaharibu uso wako''.

Image caption McGregor na Mayweather wakitambiana

Mpambano huo unatajwa kuwa miongoni mwa itakayovutia zaidi duniani.