Adnan Januzaj kujiunga na Real Sociedad

Manchester United imekubali kumuuza Adnan Januzaj kwa kitita cha pauni milioni 9.8 kwa klabu ya Hispania ya Real Sociedad. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United imekubali kumuuza Adnan Januzaj kwa kitita cha pauni milioni 9.8 kwa klabu ya Hispania ya Real Sociedad.

Manchester United imekubali kumuuza Adnan Januzaj kwa kitita cha pauni milioni 9.8 kwa klabu ya Hispania ya Real Sociedad.

Mchezaji Januzaj, mwenye umri wa miaka 22, ameambiwa kwamba anaweza kutafuta klabu nyengine msimu huu na mkufunzi Jose Mourinho.

Alishindwa kuthibitisha iwapo anafaa kundelea kuichezea manchester United wakati alipopelekwa Sunderland kwa mkopo kabla ya kuwachwa nje katika kikosi cha Mourinho kwa ziara ya maandalizi nchini Marekani.

Januzaj ambaye pia amewahi kuichezea Borussia Dortmund kwa mkopo 2015-16 anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya Jumatano.

Januzaj alijiunga na United kutoka Anderlecht wakati alipokuwa na umri wa miaka 16 na kufanikiwa kujiunga na kikosi cha kwanza cha timu hiyo 2013 chini ya ukufunzi wa David Moyes.

Akionekana mzuri kurithi nambari 11 ya mchezaji Ryan Giggs, Januzaj alitia saini kandarasi ya miaka mitano ambayo ilitarajiwa kukamilika 2018.

Real Sociedad ilimaliza katika nafasi ya sita katika ligi ya La Liga msimu uliopita na itashiriki katika mechi za kimakundi za kombe la Yuropa 2017-18