Yannick Bolassie apata makaribisho ya aina yake Tanzania

Mchezaji wa Everton Yannick Bollasie akikaribishwa na mashabiki wake nchini Tanzania
Image caption Mchezaji wa Everton Yannick Bollasie akikaribishwa na mashabiki wake nchini Tanzania

Mchezaji wa Everton Yannick Bolasie alipata mapokezi ya aina yake nchini Tanzani wakati timu hiyo ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam nchini Tanzania kwa mechi ya kirafiki.

Winga huyo wa Everton ambaye ni raia wa DR Congo na ameifungia nchi yake mabao 8 na kuichezea mara 31, alipokewa na mashabiki wake kwa shangwe wakiimba jina lake huku wakipeperusha bendera za DR Congo.

Baadaye mahabiki hao walilifuata basi la timu hiyo kwa kupanda pikipiki huku wakiendelea kuimba nyimbo za kumsifu.

Ziara hiyo ya Tanzania inalenga kusherehekea ufadhili mpya wa timu hiyo unaofanywa na kampuni ya Spotpesa kutoka Kenya.

Haki miliki ya picha Everton FC
Image caption Mashabiki wa mchezaji Yannick Bollasie wakipeperusha bendera za DR Congo

Kikosi hicho cha Ronald Koeman kinatarajiwa kuchuana na mabingwa wa Sportpesa Gor Mahia katika mechi ya kirafiki siku ya Alhamisi.

Mada zinazohusiana