Murray atupwa nje na Sam Querrey michuano ya Wimbledon

Muray hakua katika hali nzuri katika hatua za mwisho za mpambano dhidi ya QUerrey
Image caption Muray hakua katika hali nzuri katika hatua za mwisho za mpambano dhidi ya QUerrey

Bingwa mtetezi wa michuano ya Wimbledon Andy Murray amesukumwa nje ya mashindano hayo na Sam Querrey katika hatua ya nusu fainali.

Murray ambaye amekuwa na majeraha hakuweza kucheza vizuri katika mpambano huo.

Querrey, 29, ameshinda kwa seti 3-6 6-4 6-7 (4-7) 6-1 6-1 na kuwa Mmarekani wa kwanza kufanya hivyo tokea Andy Roddick alipofika katika hatua hiyo mwaka 2009.

Image caption QUerrey alikuwa katika kiwango bora kwenye mchezo huo

Murray, 30, aliongoza awali lakini maumivu ya goti yalimfanya ashindwe kuuhimili mchezo.

Majeraha aliyoyapata pia Novak Djokovic yanamfanya Murray aendelee kushikilia namba moja.

Djokovic namba mbili kwa ubora duniani, alipaswa kushinda mchezo dhidi ya Tomas Berdych lakini majeraha ya kiwiko yakakatisha matumaini hayo.