Rooney: Mechi dhidi ya Gor Mahia itakuwa ngumu

Wayne Rooney Haki miliki ya picha Everton Fc
Image caption Wayne Rooney

Wayne Rooney amesema kuwa anatarajia mechi ngumu dhidi ya Gor Mahia saa chache kabla ya kipute hicho kuanza katika uwanja wa kitafa wa Dar es Salaam.

Kulingana na mtandao wa runinga ya Citizen nchini Kenya ,nahodha huyo wa zamani wa Uingereza na mfungaji wa mabao mengi zaidi ambaye alijiunga tena na klabu yake ya utotoni Everton Wayne, kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya kuichezea Manchester United kwa takriban miaka 13 alipata makaribisho ya kipekee katika mji wa kibiashara nchini Tanzania Dar es Salaam.

''Ninafurahia kuwa nchini humu na natumai mechi hii itakuwa na mbwembwe za kila aina na kuwavutia mashabiki''

Kulingana na mtandao huo mkufunzi wa Everton Ronald Koeman aliwasili nchini Tanzania na kikosi chake chote lakini Ross barkley, Ramiro Funes ,Joel Roble wote wana majereha.

Kipa Jordan Pickford na sandro ramirez pia hawako katika ziara hiyo baada ya wawili hao kuongezewa likizo baada ya kushiriki katika mashindano ya wachezaji wasio na zaidi ya umri wa miaka 21