Nwankwo Kanu: Tusinyamazie maradhi ya moyo tena Afrika

Nwankwo Kanu: Tusinyamazie maradhi ya moyo tena Afrika

Nyota wa soka wa zamani wa Nigeria Nwankwo Kanu alikabiliana na matatizo ya moyo wakati wa uchezaji wake na anasema wakati umefika kwa hatua kuchukuliwa kuhusu maradhi ya moyo uwanjani na nje ya uwanja.

Anapanga kujenga hospitali ya moyo ya $17 milioni mjini Abuja, Nigeria. Anataka pia kujenga hospitali nyingine kama hiyo katika nchi nyingine za Afrika - moja mashariki, kaskazini na kusini mwa Afrika.

Suala la maradhi ya moyo Afrika limemshughulisha Kanu sana siku hizi, baada yake kustaafu uchezaji soka.

Ana Wakfu wa Moyo wa Kanu ambao umefanikisha upasuaji wa wagonjwa wa moyo 538 England, India, Nigeria na Israel.