Gerard Deulofeu: Barcelona wamnunua tena kutoka Everton

Gerard Deulofeu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gerard Deulofeu alikuwa anajifunza uchezaji Barcelona baada ya kujiunga na akademi yao akiwa na miaka tisa

Barcelona wamemnunua tena winga Gerard Deulofeu kutoka Everton baada ya kutumia kifungu cha kumchukua tena ambapo inadaiwa wamelipa takriban euro 12m (£10.6m).

Ametia saini mkataba wa miaka miwili.

Deulofeu awali alikwenda Everton kwa mkopo mwaka 2013-14 kisha akatia saini mkataba wa kudumu wa £4.3m mwaka 2015.

Mchezaji huyo wa miaka 23 alichezea Everton mechi 13 msimu uliopita kabla ya kujiunga na AC Milan kwa mkopo Januari kwa miaka miwili.

Mhispania huyo alikuwa kwenye akademi ya Barca Nou Camp.

Baada ya kufana msimu wa kwanza Merseyside, Deulofeu alitengwa na meneja Ronald Koeman ambaye alimkubalia kwenda Italia kipindi cha pili cha msimu.

Alianza mechi 36 akiwa Everton, na nyingine 39 akaanza akiwa kwenye benchi ambapo kwa jumla aliwafungia mabao manane.

Mkataba wake Everton ulikuwa unamalizika Juni 2018.

However Deulofeu anakabiliwa na changamoto ya kupata nafasi ya kucheza Barca, ikizingatiwa kwamba wana washambuliaji wengi stadi wakiwemo Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar.

Mada zinazohusiana