Costa na Matic wawachwa nje ya kikosi cha Chelsea

Nemanja Matic na Diego Costa kulia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nemanja Matic na Diego Costa kulia

Diego Costa na Nemanja Matic watakosa ziara ya maandalizi ya msimu ujao huko mashariki huku kukiwa na madai kwamba wawili hao wataondoka Stamford Bridge.

Chelsea inaelekea China siku ya Jumatatu na mkufunzi Antonio Conte amewaambia wachezaji wote wawili hawatachaguliwa katika kikosi cha Chelsea.

Mshambuliaji Costa mwenye umri wa miaka 28 anataka kurudi Atletico Madrid , hata ijapokuwa wamepigwa marufuku kushiriki katika uhamisho.

Manchester United imekuwa ikijaribu kumsajili Matic mwenye umri wa miaka 28.

Hatahivyo ,kuna madai kwamba baadhi ya vilabu kutoka Itali vinamtaka raia huyo wa Serb.