Federer atwaa taji la Wimbledon

Roger Federer Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Roger Federer mshindi mara nane wa michuano ya wazi ya Wimbledon

Mchezaji namba tano kwa ubora wa mchezo tenesi Roger Federer ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji la michuano ya Wimbledon, kwa mara nane.

Federer ametwaa taji hilo la Grand Slam baada ya kumshinda mpinzani wake Marin Cilic, kwa jumla ya seti tatu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Roger Federer akiwa na Marin Cilic baada ya mchezo kumalizika

Katika seti ya kwanza bingwa huyu wa kihistoria alishinda kwa 6-3, kisha akashinda kwa 6-1 na kumaliza kwa 6-4, katika mchezo ulichezwa kwa muda wa saa moja na na dakika 41.

Hili ni taji la 19 la Grand Slam, kwa mchezaji huyu raia wa Switzerland, na kuwa mchezaji mkubwa zaidi kutwaa mataji yote ya michuano ya wazi ya England.